MH LEMA AFUNGUKA HAYA



Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amekuja na staili mpya katika ulingo wa kisiasa mara hii akihimiza ushirikiano wa wapinzani kudai utawala bora.

Lema amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kumbizi ya miaka 50 ya Azimio la Arusha mjini hapa, akisema huu ni wakati wa vyama vya upinzani kushirikiana.

Lema alisema amehudhuria mkutano huo kutokana na kampeni ya ushirikiano wa vyama vyote vya upinzani waliokubaliana kupinga mwenendo wa Serikali.

 “Mkiwa na mkutano semeni niwaalike na wanachama wa Chadema waje wawape ushirikiano, lengo letu ni kuhakikisha haki inatendeka bila matabaka ya walionacho na wasionacho wala makabila,” amesema.

Katika mkutano huo, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumzia ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa na kusema kuna idadi kubwa ya kampuni za uwekezaji ambazo zinafanya hivyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI