SKENDO ZAMPA STRESS DAVIDO


MKURUGENZI wa Lebo ya HKN, David Adeleke ‘Davido’ amekimbizwa hospitali na kulazwa huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ‘stress’. Tukio hilo limejiri juzikati ambapo inaelezwa kuwa, Davido amekuwa akisumbuliwa na skendo inayozidi kuenea kwa kasi kuhusiana na kuzaa na mwanamke anayefahamika kama Ayomide Labinjo.

Haikuelezwa hasa hospitali ipi amelazwa lakini kupitia Mtandao wa Snaptchat, Davido liweka kipande cha video akiwa ametundukiwa dripu na kuwaambia mashabiki wake wamuombee.

Hivi karibuni, Ayomide alizungumza na Jarida la Punch na kuanika kila kitu kuwa, amezaa na Davido baada ya kulazimishwa wasitumie kinga.

“Kama Davido unanisikiliza ulijue hili kuwa uligoma kutumia kinga,” Ayomide aliliambia Punch. Tayari, Ayomide kwa kushirikiana na mama yake wameshafungua mashtaka yakumtaka Davido ashiriki katika malezi ya mtoto huyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI