HATMA YA WEUSI NA CHRISTIAN BELLA YAJULIKANA
Mwaka jana, collabo ya kundi la Weusi na
Christian Bella ilivuja lakini ikaja kubainika kuwa
wameingia tena studio kuifanya upya na
kuiboresha zaidi ili kuiachia rasmi.
Hata hivyo, Weusi wameonesha kuiweka benchi
bado ngoma hiyo baada ya wiki hii kuachia
wimbo mwingine, Ya Kulevya. Nick wa Pili
ameelezea hatma ya collabo hiyo.
“Kazi ya Bella tuliirudia upya, ni kazi kali, ni
project kubwa itakuja muda wake ukifika na
tunataka tukitoa, tutoe audio na video kwa
pamoja,” rapper huyo alikiambia kipindi cha
Extra Fleva cha Uplands FM kinachoendeshwa
na Ergon Elly.
Kwa upande wa video ya Ya Kulevya, Nick
amesema haitachukua muda mrefu kuanza
kuonekana kwenye TV.
Maoni
Chapisha Maoni