NEY WA MITEGO ASEMA HAKUNA WA KUMBADILISHA

 Nay wa Mitego

Hatimaye msanii Nay wa Mitego mwenye 'hit song ya wapo' amefunguka baada ya kumaliza mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Dodoma na kusema hakuna atakayeweza mbadilisha mtazamo wake katika kile anachoamini

Hiyo ni baada ya Rais Magufuli kuamuru wimbo wake huo wa 'Wapo' ufunguliwe baada ya kufungiwa na BASATA huku akishauri ufanyiwe maboresho kwa kuongeza vionjo vipya.

"Nimeitikia wito wa Mhe. Waziri, nashukuru tumeongea mengi wanasema usikatae wito kataa maneno. Haikuwa kwa ubaya, hakuna cha kurekebisha kwenye wimbo wetu wa 'Wapo' ila aliyoyapendekeza Mh. Rais nitayafanyia kazi. Huu ni wimbo wenu mashabiki wangu wote Tanzania na duniani kote, 'Wapo' ujumbe umeanza kufika. Hakuna atakae badilisha mtazamo wangu".
Aliandika msanii huyo

Pamoja na hayo Nay wa Mitego amesema anawategemea sana wananchi katika ulinzi wake kwa kuwa yeye hana 'Body-guard'

"Sina mlinzi wala Bodyguard nyie ndo walinzi wangu". Moja ya mstari aliyoandika Nay


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI