BILL NASS AFUNGUKA SABABU YA KUTOWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE
Je unajua sababu inayomfanya Bill Nass awe
msiri katika mahusiano yake?
Rapper huyo amefunguka sababu inayomfanya
awe hivyo. Akiongea na kipindi cha Bongo Dot
Com cha Times FM, hitmaker huyo wa Mazoea
amesema alishawahi kuwa katika mahusiano
mengi ambayo ambayo hakuwa na bahati nayo.
“Nimekuwa kwenye mahusiano mengi ambayo
sikuwa na bahati nayo pia inaweza
kukutengeneza kisaikolojia kutokana na mambo
ambayo nayaona kwa rafiki zangu. Nina bahati
ya kuona hivyo vitu kwa hiyo sijui huko mbele
mahusiano ni suala la feelings,” amesema rapper
huyo.
Bill ameongeza kwa sasa hana mahusiao na
mrembo yoyote wala hajawahi kufikiria kuoa hivi
karibuni.
Maoni
Chapisha Maoni