HUSSEIN MACHOZ AELEZEA SABABU YA KUFICHA MAHUSIANO YAKE
Hussein Machozi ni msiri mkubwa kwa sasa
katika ile sekta mashuhuri ya malavidavi.
Mkali huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa
akiishi nchini Italia amesema sababu kubwa ya
kutoyaweka sana mahusiano yake hadharani ni
kutokana na kuamua kuyaweka pembeni na kazi
zake.
“Kiukweli ni kwamba yupo, lakini huwa sipendi
kuweka mahusiano yangu hadharani. Muziki
wangu hauhusiani kabisa na mahusiano yangu.
Hayo ni maisha yangu kabisa binafsi,” Machozi
alimjibu shabiki kwenye video aliyoiweka
Instagram.
“Hata mwenyewe ambaye niko naye huwa
hapendi hata kutokea kwenye gazeti, hanaga
social network,” aliongeza.
Muimbaji huyo hivi karibuni amepanga kuachia
wimbo wake mpya baada ya kuwa kimya kwa
muda.
Maoni
Chapisha Maoni