MOSES IYOBO ASEMA HAWEZI KUACHA KUNENGUA



MNENGUAJI wa kundi la Wasafi Classic (WCB), Moses Iyobo, amesema hajawahi kufikiria kuwa mwimbaji kwakuwa ni kazi inayohitaji kutumia akili nyingi tofauti na unenguaji.

Iyobo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uchezaji, amesema ataendelea kubaki kuwa mnenguaji katika maisha yake yote sambamba na kuwa mwalimu kwa wenzake.

Alisema kazi ya kuimba inahitaji akili nyingi ili kufikia malengo hivyo ataendelea kubaki na kazi yake ya unenguaji.

“Nitabaki kuwa dansa maisha yangu yote, labda nitakachoongeza hapo ni kuwa mwalimu na kuwafundisha wengine, unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe. Sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,” alisema Iyobo ambaye ni mpenzi wa msanii Aunt Ezekiel.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI