FIFA YAMFUNGIA MESS MECHI NNE
Shirikisho la soka duniani FIFA March 28,
limetangaza kumfungia mechi 4, nahodha wa
timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC
Barcelona ya Hispania, Lionel Messi kwa kosa la
kutoa maneno machafu kwa mwamuzi katika
mchezo dhidi ya Chile,Machi 24.
Messi alipewa kifungo hicho saa sita kabla ya
mchezo dhidi ya Bolivia. Pia amepigwa faini ya
Paundi 8,100.
Messi alionekana kukasirika katika mchezo huo
dhidi ya Chile baada ya mwamuzi msaidizi
Marcelo van Gasse kuinua kibendera akiashiria
mchezaji huyo kumfanyia madhambi mpinzani.
Messi alirusha mkono wake juu na kumbwatukia
mwamuzi huyo kwa kusema ‘la concha de tu
madre’, kwa tafsiri ya “f*** off, your mother’s
****’ . .
Baada ya mchezo kumalizika kwa Argentina
kushinda 1-0 kwa goli la Lionel Messi, nahodha
huyo alikataa kumpa mkono mwamuzi huyo
msaidizi.
Na hizi ndio mechi ambazo atakosa Messi ni zile
za ushindani ambazo zote ni za kufuzu kombe la
Dunia.
Mechi hizo ni
March 28 – Bolivia (A)
August 28 – Uruguay (A)
September 5 – Venezuela (H)
October 2 – Peru (H)
Maoni
Chapisha Maoni