WANAFUNZI WAKUMBWA NA MAPEPO SHULENI


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imesela,
iliyopo Kata ya Imesela, Wilaya ya Shinyanga,
wamekuwa wakipiga kelele shuleni bila sababu
huku taarifa zilizopatikana shuleni hapo
Jumatano hii zinasema kwamba, wanafunzi hao
wamekuwa wakianguka na kupiga kelele, tangu
Januari mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo, walimu wa shule hiyo
wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwatuliza
na hivyo kupoteza muda wa kuingia madarasani.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi
252, Seleman Kalavina, alithibitisha uwepo wa
tukio hilo na kusema wanafunzi kila
wanapoanguka, huwa wanapiga kelele na
kutamka maneno yasiyoeleweka.
Alisema jitihada mbalimbali zimekuwa
zikifanyika ikiwemo kuwaita viongozi wa dini,
lakini tatizo hilo bado halijatatuliwa.”Hali hii
inatutisha hata sisi walimu kwani hatufundishi
kwa vile tunatumia muda mwingi kuzima
mapepo. Umefika wakati walimu wanatamani
kuhama katika shule hii.”
“Kwa ujumla, hali hii inawakumba wanafunzi wa
kike peke yao na mauzauza huanza kila siku saa
moja na nusu asubuhi mpaka muda wa masomo
unapomalizika mchana,” alisema mwalimu mkuu
huyo alipokuwa akizungumza mbele ya wajumbe
wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
waliotembelea shule hiyo.
Naye Mratibu wa Elimu, Kata ya Imesela, Julius
Wamba, alisema mauzauza katika shule hiyo
yameongezeka kuanzia Machi mwaka huu. “Hali
imezidi kuwa mbaya kuanzia Machi mwaka huu
na watoto wanapokuwa wakipiga kelele,
huwataja baadhi ya watu wanaowasababishia
hali hiyo,kutokana na hali hiyo, tumeshaita
masheikh na walokole, lakini wakiondoka tu,
mapepo yanawarudia tena na wanafunzi
wanashindwa kusoma.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI