SABABU AMBAZO WATU HUKWEPA UONGOZI
Habari ndugu msomaji wa makala zangu tazama leo ni siku nyingine kabisa ambayo tunakutana katika safu hii,leo tutakuwa tunazungumzia kwanini watu wengi wanakataa kuwa viongozi wakati hata Mungu amesema kuwa nimewaumba wanaadam wakatawale dunia,basi kupitia makala haya leo tutaangalia kwanini wengine hukataa majukumu hayo
Hebu angalia fursa itakayobadilisha maisha yako 2017 bofya hapa
1. WATU WENGI HAWAJUI KUWA WAO NI VIONGOZI
Kitu ambacho watu wengi hawafahamu kuwa mwanadam ni kiongozi kwa asili yani Mungu alishamuumba kila mwanadamu ndani yake kuna chembechembe za uongozi sasa watu wengi huwa hawalijui hilo,ndio maana mnaweza kuwa mko kwenye kikundi chochote mkamchagua mtu kuwa kiongozi akawaambia yeye hawezi,hii yote ni kuwa wanadam wengi hawatambui kuwa wao ndani yao kuna nguvu ya kuiongozi,rafiki wewe ni kiongozi na unapaswa kuongoza kwa njia yoyote ile haijalishi unaumri gani wala uko wapi ukipewa madaraka ya kuongoza wewe uongoza tu
2. WATU WENGI WANAHOFU KUWA WATATUHUMIWA NA KUCHUKIWA
Ukiangalia moja ya sababu ambayo huwafanya watu wengi sana kukataa uongozi ni kukataa kushutumiwa huwa kwa lugha nyepesi wanakataa lawama,lakini mimi naweza kusema kuwa ili uweze kufanikiwa lazima ujitahidi kuwa kiongozi popote usiogope lawama maana muda Fulani lawama ni kama shule.
3. WATU HUFIKIRIA KUWA WAO HAWANA SIFA ZA KUONGOZA
Idadi kubwa ya watu linapokuja swla la kuwaongoza watu huwa wanaona kama wao hawna sifa za kuongoza watu wengine,lakini leo nataka nikwambie kitu kimoja rafiki fanya unavyojua kwenye hii dunia ili uweze kufika mbali kuwa kiongozi na ukipewa nafasi popote ya kuongoza basi wewe uongoza tu wala usiogope hakuna aliezaliwa anajua wote tumejifunza hapahapa duniani na lazima ujue sehem pekee ya kujifunza mambo ni hapa hapa duniani
4. WATU WENGI HAWAPENDI KUCHUKIWA
Ukiangalia viongozi wengi kuna watu huwachukia na hasa unapokuwa kiongozi mtenda haki,unapotenda haki sana watu lazima watakuchukia hasa wale ambao mamabo yao hayako sawa kwaiyo watu wengine wanaogopa kitu hicho wanaogopa kuchukiwa na watu ndio maana unaona kuwa wanagoma kuwa viongozi,kitu kimoja ambacho napenda nikushauri rafiki unapokuwa kiongozi usiogope kchukiwa hakuna mafanikio yanakuja bila kuchukiwa na baadhi ya watu.piga kazi songa mbele
5. WATU WENGI NI WABINAFSI
Kuna watu wengine kweli kinachowasumbua ni ubinafsi,hawako tayari kuleta mandeleo ya watu wengine na uongozi ni kupigania watu wengine,kuleta maendeleo ya watu wengine kwaiyo watu wengi hawako tayari kufaidisha wengine kwaiyo hawapendi tu kuwa viongozi,lakini ngoja nikwambie kitu uongozi unabaraka sana hasa ukiwa muadilifu jitahidi usife kabla hujawa kiongozi
Maoni
Chapisha Maoni