SITA WAFARIKI DUNIA KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI KWENYE SHIMO LA MGODI
Wachimbaji wadogo sita katika mgodi wa dhahabu kitunda uliopo wilayani sikonge mkoani tabora wamefariki baada ya kufunikwa na kifusi cha shimo la mgodi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji.
Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia jana ambapo inadaiwa kuwa wachimbaji nane ndio wanaosadikiwa kuingia katika mgodi huo na kufukiwa,juhudi za uokoaji zinaendelea kufanywa na uongozi wa halmashauri ya wilaya na hadi sasa miili mitano imetolewa na majeruhi wawili walipelekwa katika hospitali ya wilaya ya sikonge ambao mmoja kati yao amefariki na kufikisha idadi hiyo ya watu sita na mmoja akiwa bado hajatolewa.
Licha ya viongozi wa halmashauri kutaja watu nane wanaosadikiwa kuwemo ndani ya mgodi huo baadhi ya wachimbaji wanadai kuwa watu waliofunikwa ni zaidi ya hao waliotajwa.
Maoni
Chapisha Maoni