HAJI MANARA AMWAGA POVU KUHUSU TFF


Mkuu wa  Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesikitishwa na uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akidai yupo tayari kwa mapambano kwa kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa. 

Haji Manara amesema hayo baada ya kutolewa  hukumu na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa ya kumfungia kujihusisha na masuala ya soka kutokana na makosa matatu ambayo ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila kwa kudai Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa kuwa ni Wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga na la mwisho kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.

Kufuatia maamuzi hayo ya TFF Manara amefunguka haya 

"Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa, unanipa hukumu kwa makosa nisiondikiwa katika mashtaka yao..Nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu". Alisema Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram

Haji Manara amesimamishwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia kutakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni tisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI