MLELA AFJNGUKIA NEY WA MITEGO
Muigizaji wa filamu,Yusuph Mlela, amefunguka kwa kudai kuwa kama angekuwa anauwezo wa kurap angeandaa wimbo wa kumchana Nay wa Mitego.
Wawili hao waliingia kwenye mgogoro wa kutupiana maneno mtandaoni baada ya rapa Nay wa Mitego kudai wale wasanii alioandamana akiwemo Mlela kupinga filamu za nje ni mataahira.
Mlela amemtaka Nay kuacha kufuatilia mambo yasiyo muhusu na aendelee na shughuli zake za uimbaji au akae pembeni.
“Sawa mimi na yeye tunaweza tukawa hatulingani labda kiuwezo na kimaisha kwa sababu yeye anaona tayari amekwisha rizika, ndio maana namuomba tupande ulingoni ili tuheshimiane. Mimi kama ningekuwa naimba ningeingia studio nikatengeneza wimbo wa kumchana lakini kwa vile kazi zetu haziingiliani ndiyo maana nasisitiza ki Hip hop tuu tuingie ulingoni ili tuheshimiane, tuache maneno maneno,” Mlela alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.
Aidha Mlela amekanusha kauli ya kuitwa mtoto wa kike na Nay na kumgeuzia kibao kwa kudai mtu anayeisifu mvua sana huenda ikawa imemnyea ndio maana kutwa anaizungumza kauli ya kumfananisha na mwanamke.
Maoni
Chapisha Maoni