TUNDU LISSU AKOMALIA VYETI FAKE VYA BASHITE

Wakili Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi. Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia. Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema uamuzi huo wa kulifikisha mahakamani suala la Bashite umetokana na maazimio ya baraza la uongozi la chama hicho, lengo likiwa ni kulinda utawala wa sheria na uwajibikaji nchini. Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu, sakata hilo la Bashite halikupatiwa jibu kutokana na ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wote wa umma iliyokabi...