CHID BENZI AFUNGUKA MARA YA KWANZA BAADA YA KUTOKA REHAB

Rapa Chid Benz amefunguka kwa mara ya kwanza tangia atoke Rehab alikokuwa akipata matibabu ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na amewaasa vijana watu,iaji wa Tanzania kuacha kabisa mchezo huo.

Chid Benz ambaye anaonekana mwenye afya na uso wenye furaha, amesema madawa ya kulevya sio ya kuyazungumzia. Amesema kama mtu hataki kujutia maisha yake yote basi aachane na mchezo huo mara moja.

“Stay away from Drugs,wakae mbali sana na madawa ya kulevya kitu kibaya sana sitaki kuongelea sana lakini wajitahidi (Watanzania) kadri wanavyoweza wakae mbali na madawa ya kulevya ni kitu kibaya sana kinaweza kukufanya ujutie maisha yako yote“Alisema Chid Benz kwenye mahojiano yake na Muungwana TV.

Tazama hapa chini mahojiano yake yote.



Chid Benz alishawahi kuathirika na madawa ya kulevya na kupelekwa Rehab mara tatu kabla ya Afya yake kutengamaa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI