MISRI YATANGAZA HALI YA HATARI

Viongozi wa dhehebu la Coptic wamesema tukio hilo halitawatenga na jamii ya waislamu

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ametangaza miezi mitatu ya hali ya hatari nchini kote, kufuatia shambulizi la bomu ambalo limeua zaidi ya watu 40 katika makanisa mawili ya Coptic.

Jeshi litapelekwa kusaidia polisi kulinda maeneo muhimu na vikosi vya usalama vitaruhusiwa kukamatwa bila kibali cha kukamatia.

Kufuatia tukio hilo, Rais Sisi pia ametangaza kuundwa kwa baraza litakalopambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limekiri kuendesha mashambulizi hayo.

Ahmed Abdel Hady ni muislamu ambae anasema kamwe shambulio hilo halitaweza kuwagawa Wamisri.

Waislamu na Wakristo kwa pamoja wameungana nchini humo kupinga shambulizi hilo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI