RAIS KENYATA AWAOMBEA WANAFUNZI 33 WALIOPATA AJARI TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenya amewaongoza raia wa nchi hiyo jana katika kuomboleza vifo vya wanafunzi 33 vilivyotokea Wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.
Kenyatta ambaye ni mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee, aliwaomba raia wa Kenya kusimama kwa dakika moja kuomboleza na kuwaombea wanafunzi 33, walimu 2 na dereva waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jana saa tatu asubuhi.
Rais Uhuru alitoa heshima hiyo alipokuwa katika moja ya mikutano yake ya hadhara nchini humo ambapo anatetea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Maoni
Chapisha Maoni