GABO AFUNGUKA MAHUSIANO YAKE NA WEMA SEPETU


Gabo Zigamba amefunguka kwa kudai kuwa picha za kimahaba zilizozagaa mitandaoni akiwa na Wema Sepetu ni maandalizi ya kazi yao mpya na siyo mambo mengine

Muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya filamu, amedai filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Heaven Sent’ ni full mahaba ndio maana picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinawaonyesha wakawa katika hali isiyo ya kawida.

“Movie tunayoifanya na Wema iko very tomantic ndio maana hata picha zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi mashabiki zangu naanda kitu kikali sana mara mbili za jinsi wanavyonifahamu,” alisema Gabo.

Pamoja na hayo Gabo amewataka mashabiki wa filamu waendelee kuwapatia changamoto za kejeli ikiwa ni pamoja na kusisistiza kazi nzuri ili wasanii wasibweteke isipokuwa kutoa lugha za matusi

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBINU 5 KALI ZA JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA YOYOTE MREMBO NA AKUBALI

SPIKA NDUGAI AELEZEA MAANA YA NENO FALA

FAHAMU NJIA ZA KUSAIDIA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI